+ -

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ:
قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، ابْنُ جُدْعَانَ كَانَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ يَصِلُ الرَّحِمَ، وَيُطْعِمُ الْمِسْكِينَ، فَهَلْ ذَاكَ نَافِعُهُ؟ قَالَ: «لَا يَنْفَعُهُ، إِنَّهُ لَمْ يَقُلْ يَوْمًا: رَبِّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 214]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 214]

Ufafanuzi

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu Abdullahi Bin Jad'aan, na alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kikuraishi kabla ya Uislamu, Na miongoni mwa vitendo vyake vizuri ni kuwa yeye: huunganisha ndugu zake na huwafanyia wema, na hulisha chakula masikini, na mambo mengine mengi ambayo Uislamu umeyahimiza kuyafanya, nakuwa matendo haya hayatomfaa katika Akhera yake; Na hilo ni kwa sababu ya kumkufuru Mola wake, na kuwa yeye hajawahi hata siku moja kusema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi makosa yangu siku ya Kiyama.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuweka wazi utukufu na ubora wa imani, na kuwa imani ni sharti la kukubaliwa matendo yote.
  2. Kuweka wazi ubaya wa ukafiri, na kuwa ukafiri huporomosha matendo mema.
  3. Makafiri hayatawafaa matendo yao huko Akhera kwa sababu ya kutokumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.
  4. Matendo ya mwanadamu akiwa bado yupo kwenye ukafiri huandikiwa atakapo silimu na atalipwa kwa matendo hayo.