عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«كُلُّ سُلَامَى مِنَ النَّاسِ عَلَيْهِ صَدَقَةٌ، كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ تَعْدِلُ بَيْنَ الِاثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وَتُعِينُ الرَّجُلَ فِي دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْهَا أَوْ تَرْفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ، وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقَةٌ، وَكُلُّ خُطْوَةٍ تَمْشِيهَا إِلَى الصَّلَاةِ صَدَقَةٌ، وَتُمِيطُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ».
[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية: 26]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kila kiungo kwa mwanadamu kwake ni sadaka, kila siku linalochomoza jua ndani yake ukafanya uadilifu kati ya watu wawili hiyo ni sadaka, na ukamsaidia mtu katika kipando chake ukambeba au ukamnyanyulia mzigo ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kila hatua unayopiga kwenda msikitini ni sadaka, na ukiondoa udhia barabarani nisadaka".
[Sahihi] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية - 26]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.