+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ المَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2222]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2222]

Ufafanuzi

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilifu na kwa sheria ya Muhammadi. nakuwa atavunja misalaba wanayoitukuza wakristo, nakuwa Issa amani iwe juu yake ataua nguruwe, Na pia amani iwe juu yake ataweka kodi (Jizia) na atawaamrisha watu wote kuingia katika Uislamu. Nakuwa mali itaenea na hatoikubali yeyote; na hii ni kwa sababu ya wingi wake, na kwa kutosheka kila mmoja na kile anachokimiliki mkononi mwake, na kuteremka kwa baraka na heri nyingi zenye kufuatana.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumethibitishwa kuteremka kwa Issa amani iwe juu yake zama za mwisho, nakuwa tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
  2. Sheria ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haitofutwa na sheria yoyote.
  3. Kuteremka kwa baraka katika mali zama za mwisho, na watu kutoipenda.
  4. Habari njema ya kubakia kwa dini ya Uislamu kiasi ambacho Issa amani iwe juu yake atawahukumu watu zama za mwisho.