عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: نَامَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حَصِيرٍ، فَقَامَ وَقَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ، لَوِ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً، فَقَالَ:
«مَا لِي وَلِلدُّنْيَا، مَا أَنَا فِي الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا».
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2377]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alilala Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mkeka, akasimama mkeka ukiwa umemuathiri katika ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro: Akasema:
"Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini ya mti kisha akaondoka akauacha".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2377]
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilala juu ya busati dogo lililoshonwa kutokana na baadhi ya mimea, akasimama ukiwa tayari mkeka umeathiri katika ngozi ya ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro laini basi ingelikuwa bora kuliko kujilaza kwako juu ya mkeka mgumu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sina mapenzi wala hamu ya dunia mpaka niwe na tamaa nayo, kwani mfano wangu mimi na kubakia katika dunia ni kama msafiri aliyejikinga kivulini kwa muda mfupi kisha akaondoka akakiacha.