عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:
مَا أَكَلَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْلَتَيْنِ فِي يَوْمٍ إِلَّا إِحْدَاهُمَا تَمْرٌ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6455]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6455]
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kwamba watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kula milo miwili kwa siku moja isipokuwa mlo mmoja kati ya hiyo utakuwa ni tende.