عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ:
مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاَثَ لَيَالٍ تِبَاعًا، حَتَّى قُبِضَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5416]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:
Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5416]
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.