عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا يَشْكُرُ اللَّهَ مَنْ لَا يَشْكُرُ النَّاسَ»
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد] - [سنن أبي داود: 4811]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu"
[Sahihi] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد] - [سنن أبي داود - 4811]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kwa kawaida hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu kwa wema na mazuri waliyomfanyia, na hii ni kwa sababu mambo haya mawili yote yanaungana, kiasi kwamba katika tabia yake na desturi yake ni kukufuru neema na kuacha kushukuru, pia atakuwa katika kawaida yake ni kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na kupuuza katika kushukuru kwa neema hizo.