عن عرفجة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: "من أتاكم وأمرُكُم جَمِيْعٌ على رجل واحد، يُريد أن يَشُقَّ عَصَاكُم، أو يُفَرِّقَ جَمَاَعَتَكُم، فاقتُلُوهُ".
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa A'rfaja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote Atakayekujieni na akakuamrisheni nyote muwe dhidi ya mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, na usambaratishe umoja wenu, basi muuweni".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Lengo la hadithi hii ni katika kupambana na watu waovu, na anayetaka kusambaratisha umoja wa waislamu baada kukusanyika kwao na kumtii kwao kiongozi, na imeonyesha kuwa waislamu wakikubaliana juu ya kiongozi mmoja, kisha akaja anayetaka kumuondoa kiongozi wao ambaye wao wamekubaliana juu yake, ni wajibu kwao wamsimamishie sheria hata kama ni kwa kumuua; kwaajili ya kuzuia shari zake na kulinda damu za waislamu.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. uwajibu wa kusikia na kutii kwa kiongozi wa waislamu, na uharamu wa kutoka dhidi yake.
  2. Atakayejitoa kwa kiongozi ambaye waislamu wamekubaliana kwake, basi huyo ni wajibu kumuuwa vyotevyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya juu na nasaba .
  3. Hadithi kwa muonekano wake inakusanya sawa sawa mwenye kutoka awe mmoja au kundi basi watauwawa, ikiwa huo umoja una nguvu na uwezo na wakatoka baadhi yao kwa kuleta tafsiri kuwa inafaa basi nao watakuwa waovu, ama ikiwa hawatokuwa na tasfiri na wakataka kuupindua utawala, basi hawa hukumu yao ni kama hukumu ya vibaka.
  4. Kuhimizwa juu ya kuwa pamoja na kuto farakiana na kutofautiana.