عَنْ عِكْرِمَةَ:
أَنَّ عَلِيًّا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ حَرَّقَ قَوْمًا، فَبَلَغَ ابْنَ عَبَّاسٍ فَقَالَ: لَوْ كُنْتُ أَنَا لَمْ أُحَرِّقْهُمْ لِأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ تُعَذِّبُوا بِعَذَابِ اللَّهِ»، وَلَقَتَلْتُهُمْ كَمَا قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 3017]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ikrima:
Ya kwamba Ally radhi za Allah ziwe juu yake aliwachoma watu fulani, zikamfikia taarifa Bin Abbas akasema: Lau ningelikuwa mimi nisingewachoma, kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu", na ningewaua tu kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayebadili dini yake basi muuweni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 3017]
Alijitahidi Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akawachoma watu fulani kwa moto, miongoni mwa mazandiki walioritadi kutoka katika Uislamu, zikamfikia taarifa Abdallah bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, akamuunga mkono kwa kuwauwa kwake; lakini akakemea kuwachoma kwa moto. Na akasema: Lau ningelikuwa katika nafasi yake nisingeliwachoma kwa moto; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake alibainisha kuwa haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa moto, lakini inatosha tu kuwauwa, kwani alisema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu na akabadili dini yake kwa dini nyingine basi muuweni.