عَنْ ابْنَ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِذَا رَأَيْتُمُوهُ فَصُومُوا، وَإِذَا رَأَيْتُمُوهُ فَأَفْطِرُوا، فَإِنْ غُمَّ عَلَيْكُمْ فَاقْدُرُوا لَهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1900]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1900]
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.