عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«أَحَبُّ الْبِلَادِ إِلَى اللهِ مَسَاجِدُهَا، وَأَبْغَضُ الْبِلَادِ إِلَى اللهِ أَسْوَاقُهَا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 671]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 671]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.