عَنْ جَابِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ مِنْ أَحَبِّكُمْ إِلَيَّ وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ القِيَامَةِ أَحَاسِنَكُمْ أَخْلاَقًا، وَإِنَّ أَبْغَضَكُمْ إِلَيَّ وَأَبْعَدَكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ القِيَامَةِ الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ وَالمُتَفَيْهِقُونَ»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، قَدْ عَلِمْنَا الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ فَمَا الْمُتَفَيْهِقُونَ؟ قَالَ: «الْمُتَكَبِّرُونَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2018]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya Kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: "Ni wale wenye kiburi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2018]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa wale wanaowapendeka zaidi kati yenu kwake katika dunia, na wa karibu zaidi katika kikao miongoni mwenu siku ya Kiyama, ni yule mwenye tabia nzuri zaidi yenu, na kuwa anayechukiwa zaidi miongoni mwenu kwake katika dunia, na atakayekuwa mbali zaidi miongoni mwenu katika kikao siku Kiyama ni mwenye tabia mbaya zaidi miongoni mwenu; "Wenye maneno mengi" wenye kukithirisha maneno kwa kukijilazimisha na kwa kutoka katika haki, "na wenye kuzama zaidi" wenye kuzungumza maneno kwa upana kwa kujitia ufasaha na kwa kuyatukuza maneno yao pasina kuchukua tahadhari wala kuchunga, "na wenye kujitia kujua" wakasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwisha wajua wenye maneno mengi na wenye kuzama zaidi, ni wapi wenye kujifanya kujua? Akasema: Ni wenye kiburi wenye kuwakejeli watu, wale wenye kuzungumza kwa upana katika maneno yao, na hufungua vinywa vyao kwa wingi wa maneno.