عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما مرفوعاً: قال: لم يكن رسول الله صلى الله عليه وسلم فاحشاً ولا متفحشاً، وكان يقول: «إن من خياركم أحسنكم أخلاقًا».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Na kutoka kwa Abdillahi Bin Amriy bin Aaswi- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u- Amesema: "Hakuwa Mtume rehema na Amani zimfikie Muovu, wala mwenye kutaka machafu" Na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mzuri wenu kitabia"
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Hakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- mwenye kauli mbovu, wala vitendo vibaya, wala mwenye kukusudia kufanya hayo, mwenye kujilazimisha kwa hayo, bali alikuwa mwenye tabia tukufu, na akaeleza kuwa muumini bora ni yule mwenye tabia njema kati yao, kwasababu tabia njema inapelekea katika matendo mazuri na kuacha maovu.