+ -

عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
قَدِمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَبْيٌ، فَإِذَا امْرَأَةٌ مِنَ السَّبْيِ قَدْ تَحْلُبُ ثَدْيَهَا تَسْقِي، إِذَا وَجَدَتْ صَبِيًّا فِي السَّبْيِ أَخَذَتْهُ، فَأَلْصَقَتْهُ بِبَطْنِهَا وَأَرْضَعَتْهُ، فَقَالَ لَنَا النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَتُرَوْنَ هَذِهِ طَارِحَةً وَلَدَهَا فِي النَّارِ؟» قُلْنَا: لاَ، وَهِيَ تَقْدِرُ عَلَى أَلَّا تَطْرَحَهُ، فَقَالَ: «لَلَّهُ أَرْحَمُ بِعِبَادِهِ مِنْ هَذِهِ بِوَلَدِهَا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5999]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Walikuja mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara kukawa na mwanamke miongoni mwa mateka akikamua maziwa yake na kunyonyesha, akipata mtoto katika mateka anamchukua, anamkumbatia na kumuweka tumboni kwake na kumnyonyesha, basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kutuambia: "Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni?" Tukasema: Hapana, hawezi kumtupa, akasema: "Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5999]

Ufafanuzi

Waliletwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika kabila la Hawazini, mara kukawa na mwanamke miongoni mwao akimtafuta mwanaye, kila akipata mtoto anamnyonyesha kwa sababu ya kudhurika kwake kwa wingi wa maziwa katika matiti yake, mara, akampata mwanaye katika mateka akamchukua, akamkumbatia tumboni kwake na akamnyonyesha, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwaambia Maswahaba zake: Hivi mnadhani mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanaye motoni? Tukasema: Kamwe, hawezi kumtuka kwa hiyari yake milele. Akasema: Basi Mwenyezi Mungu ana huruma zaidi kwa waja wake Waislamu kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Huruma pana ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba yeye anawatakia mema na Pepo, na kusalimika na Moto.
  2. Kunufaika na matukio na kuyafungamanisha na kutoa maelekezo na mafunzo.
  3. Inampasa muumini awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu, na wala asikate tamaa, ikiwa ni pamoja na kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na msimamo katika dini yake, kwani Yeye Mtukufu Ndiye Mwenye huruma pana zaidi.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama
Ziada