+ -

عن أنس بن مالك رضي الله عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمُعَاذٌ رَدِيفُهُ عَلَى الرَّحْلِ قَالَ: «يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، قَالَ: «يَا مُعَاذُ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، ثَلَاثًا، قَالَ: «مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللهُ عَلَى النَّارِ»، قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَفَلَا أُخْبِرُ بِهِ النَّاسَ فَيَسْتَبْشِرُوا؟ قَالَ: «إِذًا يَتَّكِلُوا». وَأَخْبَرَ بِهَا مُعَاذٌ عِنْدَ مَوْتِهِ تَأَثُّمًا.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 128]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto", akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je, niwaeleze watu ili wapate habari njema? Akasema: "Ukifanya hivyo, watabweteka". Na alieleza Muadhi jambo hili wakati wa kifo chake kwa kuogopa kupata dhambi za kuficha elimu.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 128]

Ufafanuzi

Alikuwa Muadhi bin Jabali -Radhi za Allah ziwe juu yake- amepanda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya mnyama wake, akamuita: Ewe Muadhi? Akarudia wito mara tatu; Kwa kusisitiza umuhimu wa yale atakayomueleza.
Na mara zote hizo Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akimjibu kwa kusema: "Labaika kwa heshima yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Yaani: Nimekujibu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jibu moja moja, na ninataka utukufu kwa kukujibu wewe.
Akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hakuna yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuaubudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isopokuwa Allah, na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa ukweli toka moyoni mwake, si muongo, ikiwa atakufa katika hali hii basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni.
Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- awaeleze watu ili wafurahi na wajipe bishara njema?
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akachelea watu kubweteka katika hilo, na wapunguze kufanya matendo.
Muadhi hakumsimulia hilo yeyote ila kabla ya kifo chake; kwa kuhofia kuingia katika dhambi za kuficha elimu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda kinaadiga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumpakiza kwake Muadhi nyuma ya mnyama wake.
  2. Njia ya ufundishaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba alirudia rudia wito kwa Muadhi ili akaze usikivu wake kwa yale atayoyazungumza.
  3. Katika sharti za shahada: Ya Kushuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni awe msemaji wake ni mkweli na yakini, asiwe muongo au na shaka.
  4. Watu wa tauhidi hawatokaa milele katika moto wa Jahannam, hata kama watauingia kwa sababu ya madhambi yao; watatolewa baada ya kusafishwa.
  5. Fadhila za shahada mbili kwa atakayezisema akiwa mkweli.
  6. Kufaa kuacha kuzungumza baadhi ya mazungumzo katika baadhi ya hali, yatakapoambatana na madhara.