عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ:
جَاءَتْنِي مِسْكِينَةٌ تَحْمِلُ ابْنَتَيْنِ لَهَا، فَأَطْعَمْتُهَا ثَلَاثَ تَمَرَاتٍ، فَأَعْطَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا تَمْرَةً، وَرَفَعَتْ إِلَى فِيهَا تَمْرَةً لِتَأْكُلَهَا، فَاسْتَطْعَمَتْهَا ابْنَتَاهَا، فَشَقَّتِ التَّمْرَةَ الَّتِي كَانَتْ تُرِيدُ أَنْ تَأْكُلَهَا بَيْنَهُمَا، فَأَعْجَبَنِي شَأْنُهَا، فَذَكَرْتُ الَّذِي صَنَعَتْ لِرَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «إِنَّ اللهَ قَدْ أَوْجَبَ لَهَا بِهَا الْجَنَّةَ، أَوْ أَعْتَقَهَا بِهَا مِنَ النَّارِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2630]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Alinijia mwanamke mmoja Masikini akiwa amebeba mabinti zake wawili, nikawalisha tende tatu, akawapa kila mmoja wao tende moja, kisha akanyanyua tende moja ili kuitumia , akawalishi mabinti zake kwa kuigawa tende ile vipande viwili, ambayo alihitaji kuila mwenyewe, kikanistaajabisha kitendo chake hicho, nikamueleza Mtume alicho kifanya mwanamke yule, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2630]
Ameeleeza mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba mwanamke moja masikini alimjia akiwa kawabeba watoto wake wa kike wawili, akamuomba chakula, akampatia tende tatu, akampatia kila mmoja miongoni mwa mabinti zake tende moja ili ale, watoto wake wakaihitaji tende ile mmoja aliyotaka kuila, akawakatia tende ile vipande viwili, jambo hilo likamshanga mno Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akakieleza kitendo alichokifanya mwanamke yule kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu kamuwajibishia Pepo kwa tende hii, au kamuacha huru na Moto.