+ -

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّمَا مَثَلُ الْجَلِيسِ الصَّالِحِ وَالْجَلِيسِ السَّوْءِ كَحَامِلِ الْمِسْكِ وَنَافِخِ الْكِيرِ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ: إِمَّا أَنْ يُحْذِيَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا طَيِّبَةً، وَنَافِخُ الْكِيرِ: إِمَّا أَنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ رِيحًا خَبِيثَةً».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2628]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
“Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma. Mbeba miski: atakukaribia utapata harufu nzuri ya marashi yake, au utanunua kwake, na ama mfua vyuma: Ima atachoma nguo zako, au utasikia harufu mbaya.”

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2628]

Ufafanuzi

Amepiga mfano Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wa aina mbili za watu:
Aina ya kwanza: Rafiki mwema anayemjulisha rafiki yake kwa Mwenyezi Mungu na yanayomridhisha, na kumsaidia katika utiifu, Mfano wake ni kama muuza miski, ima atakupa, au utanunua kwake, au utapata na kunusa harufu nzuri kutoka kwake.
Aina ya pili: Rafiki na swahiba mbaya; Anayeziba njia ya Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika kutenda maasi, na unaona wazi kwake matendo machafu, na wewe unasemwa vibaya kwa kufuatana naye na kukaa na mtu kama yeye. Mfano wake ni kama mhunzi apulizaye moto wake; ima itachoma nguo zako kutokana na cheche zake zinazoruka, au utasikia harufu mbaya kwa kukaa karibu naye.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inaruhusiwa kutumia mifano ili kusogeza maana karibu kwa msikilizaji.
  2. Himizo na hamasisho kwa watu kuwa pamoja na watu watiifu na waadilifu, na kujiepusha na watu waovu na wenye maadili mabaya.