عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ عَالَ جَارِيَتَيْنِ حَتَّى تَبْلُغَا جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَنَا وَهُوَ» وَضَمَّ أَصَابِعَهُ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2631]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2631]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeruzukiwa mabinti wawili au dada wawili, akawasimamia katika mahitaji na malezi na kuwaelekeza katika kheri na kuwatahadharisha na shari na mfano wa hayo mpaka wakakua na kubalehe; atakuja siku ya Kiyama akiwa yeye na Mtume rehema na amani ziwe juu yake mfano wa hivi viwili, akaunganisha vidole vyake viwili, kidole cha shahada na cha kati.