عن عبد الله بن زيد بن عاصم المازني رضي الله عنه قال: (شُكِيَ إلى النبيِّ صلى الله عليه وسلم الرَّجلُ يُخَيَّلُ إِليه أنَّه يَجِد الشَّيء في الصَّلاة، فقال: لا ينصرف حتَّى يَسمعَ صَوتًا، أو يَجِد رِيحًا).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin zaidi bin A'swim Al-maaziniy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "paliletwa mashtaka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayepata wasiwasi kuwa anapata kitu ndani ya swala (katika vitenguzi vya udhu), Akasema: asiondoke mpaka asikie sauti, au apate harufu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Hadithi hii (kama alivyoeleza Imamu An nawawiy) -Mwenyezi Mungu amrehemu- ni katika kanuni kuu za uislamu na msingi wake ambao hukumu nyingi tukufu zinajengeka juu yake, nayo ni kubaki vitu vilivyo na uhakika katika hukumu yake, haivuki hapo kwasababu tu ya dhana na shaka, sawa sawa shaka iwe na nguvu au isiwe na nguvu, madamu tu haijafika katika ngazi ya uhakika au dhana kuzidi, na mifano ya hilo ni mingi haifichikani, na miongoni mwake ni hadithi hii, madamu mtu ana uhakika na twahara yake, kisha akapata shaka katika kutenguka kwa twahara yake, basi asili ni kubakia kwa twahara yake, na kinyume chake pia, atakayekuwa na uhakika wa hadathi (kutokuwa na udhu) na akawa na shaka na twahara yake, basi kimsingi ni kubakia kwa hadathi yake (kutokuwa na udhu) na katika hili zinaingia nguo na maeneo, asili yake ni twahara, isipokuwa kwa uhakika wa unajisi wake, na katika hilo pia ni idadi ya rakaa za swala, atakayekuwa na uhakika kuwa ameswali rakaa tatu kwa mfano, na akawa na shaka na rakaa ya nne, asili ni kutokuwepo kwa rakaa hiyo, na atatakiwa aiswali hiyo rakaa ya nne, na katika hili pia ni yeyote atakayekuwa na shaka katika kumtaliki mke wake, basi kimsingi ni kubaki kwa ndoa, na hivyo hivyo katika maswala mengi ambayo hayafichikani.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama