عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِذَا رَأَى أَحَدُكُمُ الرُّؤْيَا يُحِبُّهَا فَإِنَّهَا مِنَ اللَّهِ، فَلْيَحْمَدِ اللَّهَ عَلَيْهَا وَلْيُحَدِّثْ بِهَا، وَإِذَا رَأَى غَيْرَ ذَلِكَ مِمَّا يَكْرَهُ، فَإِنَّمَا هِيَ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَلْيَسْتَعِذْ مِنْ شَرِّهَا، وَلاَ يَذْكُرْهَا لِأَحَدٍ، فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 7045]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 7045]
Ameeleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa ndoto njema yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaeleza amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na akiota yanayomchukiza na kumhuzunisha basi hayo yanatokana na Shetani; aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na wala asimsimulie yeyote; kwani ndoto hiyo haitomdhuru, kwani Mwenyezi Mungu ameyafanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na kero zinazoambatana na ndoto.