+ -

عن جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعَلِّمُنَا الِاسْتِخَارَةَ فِي الْأُمُورِ كَمَا يُعَلِّمُنَا السُّورَةَ مِنَ الْقُرْآنِ، يَقُولُ: «إِذَا هَمَّ أَحَدُكُمْ بِالْأَمْرِ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الْفَرِيضَةِ، ثُمَّ لِيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ وَأَسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وَأَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ الْعَظِيمِ، فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلَا أَقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلَا أَعْلَمُ، وَأَنْتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الْأَمْرَ خَيْرٌ لِي فِي دِينِي، وَمَعَاشِي، وَعَاقِبَةِ أَمْرِي» أَوْ قَالَ: «عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ، فَاقْدُرْهُ لِي وَيَسِّرْهُ لِي ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ، وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّ هَذَا الْأَمْرَ شَرٌّ لِي فِي دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي» أَوْ قَالَ: «فِي عَاجِلِ أَمْرِي وَآجِلِهِ، فَاصْرِفْهُ عَنِّي وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِي الْخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أَرْضِنِي» قَالَ: «وَيُسَمِّي حَاجَتَه».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 1162]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitufundisha kutaka uchaguzi (kwa Mwenyezi Mungu) katika mambo yetu yote kama anavyotufundisha sura katika Qur'ani, Akisema: "Atakapo dhamiria mmoja wenu kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, kisha aseme: 'Allahumma Inniy As-takhiiruka bi ilmika, wa astaq-diruka biqud-ratika wa as-aluka min fadhw-lika al-adhwiim, fa innaka taqdiru walaa aq-diru wata'alamu walaa a'alamu wa anta allaamul ghuyuub, Allahumma inkunta ta'alamu anna haadhal amru- na atataja jambo lenyewe -Khairun lii fii diiniy wadun-yaaya wamaashii wa aaqibatu amriy (Ajiluhuu wa Aajiluhu) Faq-dirhu lii wayassirhuu lii thumma baarik liiy fiihi, wa in kunta ta'alamu anna haadhal amru sharrun lii fii diiniy wa dun yaaya wa maashiy wa Aaqibatu Amriy Fas-rif-huu anniy was-rifniiy anhu waqdir liyal khaira haithu kaana thummar-dhinii bihi" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakutaka uchaguzi kupitia elimu yako, na ninakuomba uwezo kupitia uwezo wako, na ninakuomba unipe kutoka katika fadhila zako tukufu, kwani wewe unaweza na mimi siwezi, na unajua na mimi sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyofichikana, Ewe Mola wangu ikiwa unajua kuwa jambo hili (Anataja shida yake) ni kheri kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (iwe kwa haraka au kwa kuchelewa) basi nakuomba niwezeshe na unifanyie wepesi kwangu kisha unibariki mimi ndani ya jambo hili, Na ikiwa unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liepushe nami na uniepushe nalo, kisha nipangie heri mahala popote itakapokuwa kisha niridhishe nayo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 1162]

Ufafanuzi

Muislamu akitaka kufanya jambo katika mambo ambayo hayajulikani upande ulio sawa ndani yake, basi ni sheria kwake aswali swala ya Istikhaara (ya kuomba uamuzi) kiasi kwamba alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao swala hii kama anavyowafundisha sura ndani ya Qur'ani, anaswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi kisha anamuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uchaguzi" Kwa kuomba uniongoze katika jambo lenye kheri zaidi baina ya mambo mawili, na ninakuomba "Kupitia elimu yako", pana iliyozingira kila kitu, "na ninakutaka kupitia uwezo wako", wenye kutekelezeka kwani wewe hakikushindi chochote, "na ninakuomba katika fadhila zako" na wema wako "mtukufu" mpana; kwani kipawa chako ni fadhila kutoka kwako, na hakuna yeyote mwenye haki yake juu ya neema; "kwani wewe unaweza" juu ya kila kitu, na mimi ni dhaifu nisiyejiweza "na wala siwezi" jambo lolote isipokuwa kwa msaada kutoka kwako, "na" wewe "unajua" kwa elimu iliyokusanya na kuvizingira vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana, na kwa kheri na shari, "na" mimi "sijui" chochote isipokuwa kwa taufiki yako na uongofu wako, "na wewe ni Mjuzi wa mambo ya ghaibu" wewe unaelimu isiyokuwa na mipaka, na uwezo wenye kutendeka, na hakuna kwa lolote katika hayo kwa yeyote asiyekuwa wewe awezaye kufanya hayo, ila yale uliyoyapanga kwake na ukamuwezesha. Kisha muislamu atamuomba Mola wake Mlezi, na atataja haja yake, kwa kusema: " Ewe Mola wangu" hakika mimi nimekabidhi jambo kangu kwako, basi "ikiwa unajua" katika elimu yako kuwa jambo hili "hapa atalitaja" kwa mfano kama kununua nyumba, au kununua kwangu gari hili, au kumuoa kwangu mwanamke huyu au mengineyo.... Ikiwa jambo hili lilikwishatangulia katika elimu yako yakuwa ndani yake kuna "kheri kwangu katika dini yangu" ambayo ndiyo ngome ya jambo langu, "na maisha yangu" katika dunia yangu "na mwisho wa jambo langu" na hatima ya jambo langu, au alisema: "haraka ya jambo langu na kuchelewa kwake" katika dunia na Akhera; "liwezeshe" na uliandae na ulitimize "kwangu", na ulirahisishe "na ulifanye kuwa jepesi kwangu" "kisha libariki" na ukithirishe kheri "ndani yake kwangu", "na ikiwa unajua" ewe Allah "kuwa jambo hili" nililokuamba uamuzi kwalo "ni shari kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu -au alisema katika haraka ya jambo langu na kuchelewa kwake, basi liepusha nami na uniepushe nalo, na unikadirie kheri mahala popote itakapokuwa, kisha niridhishe nayo" na kwa hukumu zako zote ninazozipenda na ninazozichukia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Pupa kubwa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuwafundisha Maswahaba zake radhi za Allah ziwe juu yao swala hii; kwakuwa ndani yake kuna manufaa na kheri kubwa.
  2. Sunna ya kuomba uchaguzi na kuomba dua iliyopokelewa baada yake.
  3. Kuomba uchaguzi (Istikhaara) ni sunna katika mambo ya halali ambayo hupatikana kusitasita ndani yake, na wala haiwi katika jambo la wajibu au la sunna; kwa sababu asili ni kuyafanya, lakini inawezekana kuomba uchaguzi katika mambo yanayoambatana na hayo kama kuchagua marafiki wa kwenda nao katika Umra au Hija.
  4. Jambo la wajibu na la sunna hayaombewi uchaguzi katika kuyafanya kwake, na haramu na machukizo hayaombewi uchaguzi katika kuyaacha kwake.
  5. Ataichelewesha dua iwe baada ya swala; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Kisha na aseme", na ikisemwa kabla ya salamu pia hakuna ubaya.
  6. Ni wajibu kwa mja ayarejeshe mambo yote kwa Mwenyezi Mungu, na ni wajibu kwake ajiweke mbali na ujanja wake na nguvu zake; kwa sababu hana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu.