عَنْ صُهَيْبٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«عَجَبًا لِأَمْرِ الْمُؤْمِنِ، إِنَّ أَمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ، وَلَيْسَ ذَاكَ لِأَحَدٍ إِلَّا لِلْمُؤْمِنِ، إِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ، فَكَانَ خَيْرًا لَهُ، وَإِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ صَبَرَ، فَكَانَ خَيْرًا لَهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2999]
المزيــد ...
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2999]
Anastaajabu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, jambo na hali za muumini kwa namna ya kufurahishwa; Hii ni kwa sababu hali zake zote ni kheri, na sivyo hivyo kwa yeyote isipokuwa Muumini. Mambo mazuri yakimpata, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, analipwa kwa kushukuru. Ukimpata msiba husubiri na hutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu, na hupata malipo ya subira, hivyo anakuwa katika malipo kwa kila hali.