+ -

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ:
«إِنَّ لِلْمُؤْمِنِ فِي الْجَنَّةِ لَخَيْمَةً مِنْ لُؤْلُؤَةٍ وَاحِدَةٍ مُجَوَّفَةٍ، طُولُهَا سِتُّونَ مِيلًا، لِلْمُؤْمِنِ فِيهَا أَهْلُونَ، يَطُوفُ عَلَيْهِمِ الْمُؤْمِنُ فَلَا يَرَى بَعْضُهُمْ بَعْضًا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2838]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema:
"Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2838]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya neema za peponi, nakwamba muumini ndani ya pepo atakuwa na hema pana kwa ndani, lilitokana na madini ya lulu yenye kung'aa, upana wake na urefu wake kuelekea juu ni maili sitini, katika kila mahali na kila kona katika kona zake nne kuna wake, na wote hawaonani, muumini atakuwa akiwazungukia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa ukubwa wa neema za watu wa peponi.
  2. Himizo la kufanya amali njema kwa kubainishwa yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu kwa ajili yao miongoni mwa neema.