عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«نَارُكُمْ جُزْءٌ مِنْ سَبْعِينَ جُزْءًا مِنْ نَارِ جَهَنَّمَ»، قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ كَانَتْ لَكَافِيَةً. قَالَ: «فُضِّلَتْ عَلَيْهِنَّ بِتِسْعَةٍ وَسِتِّينَ جُزْءًا كُلُّهُنَّ مِثْلُ حَرِّهَا».

[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."

Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto wa Duniani ni sehemu moja tu kutoka katika Moto wa Jahannam, Hivyo basi moto wa Akhera ukali wake unazidi Moto wa Duniani mara sitini na tisa, kila sehemu moja ya moto huo upo sawa na ukali wa moto wa Duniani. Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika Moto wa Duniani ulikuwa unatosha kuwaadhibu waliokuwamo humo, Akasema: Moto wa Jahannam umeuzidi moto wa Duniani kwa zaidi ya mara sitini na tisa, na mara zake zote hizo sitini na tisa ni sawa na mara moja kutokana na ukali wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kunatolewa tahadhari kutoka na Moto ili watu wajiepushe na matendo yatakayo wafikisha kwenye moto wa Jahannam.
  2. Ukubwa wa Moto wa Jahannam na adhabu yake, na ukali wa joto lake.