عن المُسْتَوْرِد بن شَدَّاد رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «ما الدنيا في الآخرة إلا مِثْل ما يجعل أحدكم أُصْبُعَهُ في اليَمِّ، فلينظر بِمَ يَرْجع!».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Mustaurid bin Shaddadi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Si chochote dunia katika Akhera isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu anapoweka kidole chake baharini, kisha atazame kimerudi na nini!"
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi hii: Nikuwa utakapotaka kujua uhalisia wa dunia ukilinganisha na Akhera, basi weka kidole chako baharini kisha kinyanyue, kisha tazama kitarudi na nini?! wala hakiwezi kurudi na chochote, ukilinganisha na bahari, na hii ndio maana ya dunia ukiliganisha na Akhera katika ufupi wa muda wake na kumalizika kwa ladha zake na kudumu kwa Akhera na kudumu kwa ladha zake na neema zake isipokuwa ni kama kiwango cha maji yanayobakia katika kidole kwa maji ya bahari yaliyobakia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Si chochote starehe za dunia katika Akhera ila kidogo). Vyote ninavyowapa viumbe miongoni mwa neema za dunia na ladha zake, anastarehe nazo mja muda mfupi, zimezungukwa na vikwazo, na zimechanganyikana na matatizo, na anajipamba nazo mwanadamu muda mfupi kwa kujifaharisha na kujionyesha, kisha vinatoweka hivyo haraka mno, na yanafuatia masikitiko na majuto: (Na hamjapewa kitu chochote, (ila) hicho ni starehe za dunia na pambo lake, na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu hayo ni bora na ni yenye kubakia, hivi hamtii akilini). Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu katika neema za kudumu, na maisha ya raha, na majumba ya kifahari na furaha hayo ni bora na yenye kubakia katika sifa zake na kiwango chake, nayo ni yenye kubakia milele.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama