عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا مِنْ قَوْمٍ يَقُومُونَ مِنْ مَجْلِسٍ لَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ فِيهِ إِلَّا قَامُوا عَنْ مِثْلِ جِيفَةِ حِمَارٍ، وَكَانَ لَهُمْ حَسْرَةً».
[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 4855]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 4855]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba hakuna kundi la watu watakaokaa katika kikao kisha wakanyanyuka katika kikao hicho haliyakuwa hawajamtaja Mwenyezi Mungu ndani yake isipokuwa watanyanyuka katika mfano wa mzoga wa punda katika kunuka na uchafu; na hii ni kwa sababu walishughulika na mazungumzo wakaacha kumtaja Mwenyezi Mungu, na kikao hicho kwao kitakuwa ni masikitiko siku ya Kiyama na ni mapungufu na majuto kwao.