عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَوْ كَانَ لِابْنِ آدَمَ وَادِيَانِ مِنْ مَالٍ لَابْتَغَى وَادِيًا ثَالِثًا، وَلَا يَمْلَأُ جَوْفَ ابْنِ آدَمَ إِلَّا التُّرَابُ، وَيَتُوبُ اللهُ عَلَى مَنْ تَابَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1048]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:
"Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1048]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba lau kama mwanadamu angelipata bonde moja lililojaa dhahabu, basi angependa kwa sababu ya tamaa yake ambayo ndiyo maumbile yake awe na mabonde mengine mawili, na kwamba mwanadamu haachi kuipupia dunia mpaka anakufa na lijae tumbo lake kwa udongo wa kaburi lake.