عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إن أَهْوَنَ أهل النار عذابا يوم القيامة لرجل يوضع في أَخْمَصِ قدميه جمرتان يغلي منهما دماغه ما يرى أن أحدا أشد منه عذابا وإنه لَأَهْوَنُهُم عذابا».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Nu'man bin Bashiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika mwenye adhabu nyepesi zaidi katika watu wa motoni siku ya kiyama, ni mtu atawekewa ndani ya nyayo zake makaa mawili ya moto, utakuwa ukitokota kupitia hayo ubongo wake, na yeye atakuwa akiona kuwa hakuna mtu mwenye adhabu kali zaidi yake, na hakika kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nyepesi kuliko wao".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa hakika mtu mwenye adhabu ndogo kabisa katika watu wa motoni siku ya kiyama, ni yule atakayewekewa chini ya nyayo zake makaa mawili ya moto, utakuwa ukitokota kupitia hayo ubongo wake, na yeye atakuwa akiona kuwa ndiye mwenye adhabu kali kuliko watu wote, hali yakuwa yeye ndiye mwenye nafuu kuliko wao; kwasababu lau kama angemuona mwenzie basi angeona kuwa yeye ana nafuu, na angejiliwaza kwa hilo, lakini yeye anaona kuwa yeye ndiye mwenye adhabu kaliko watu wote, na hapo ndipo anapolalama na kuzidisha balaa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama