عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَمُرَّ الرَّجُلُ بِقَبْرِ الرَّجُلِ فَيَقُولُ: يَا لَيْتَنِي مَكَانَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake".

Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Kiyama hakitosimama mpaka mtu apite katika kaburi atamani laiti angelikuwa maiti mfano wake, na sababu ni kuihofia nafsi yake kwa kutoweka dini yake kwa kuzidiwa na batili na waovu, na kudhihiri kwa fitina na maasi na maovu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuna ishara ya kudhihiri maasi na fitina zama za mwisho.
  2. Himizo la kuchukua tahadhari na kujiandaa na mauti kwa imani na matendo mema, na kujiweka mbali na mazingira ya fitina na balaa.