عَنْ أَبٍي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَلَسَ ذَاتَ يَوْمٍ عَلَى المِنْبَرِ وَجَلَسْنَا حَوْلَهُ، فَقَالَ: «إِنِّي مِمَّا أَخَافُ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِي، مَا يُفْتَحُ عَلَيْكُمْ مِنْ زَهْرَةِ الدُّنْيَا وَزِينَتِهَا» فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَوَيَأْتِي الخَيْرُ بِالشَّرِّ؟ فَسَكَتَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقِيلَ لَهُ: مَا شَأْنُكَ؟ تُكَلِّمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلاَ يُكَلِّمُكَ؟ فَرَأَيْنَا أَنَّهُ يُنْزَلُ عَلَيْهِ؟ قَالَ: فَمَسَحَ عَنْهُ الرُّحَضَاءَ، فَقَالَ: «أَيْنَ السَّائِلُ؟» وَكَأَنَّهُ حَمِدَهُ، فَقَالَ: «إِنَّهُ لاَ يَأْتِي الخَيْرُ بِالشَّرِّ، وَإِنَّ مِمَّا يُنْبِتُ الرَّبِيعُ يَقْتُلُ أَوْ يُلِمُّ، إِلَّا آكِلَةَ الخَضْرَاءِ، أَكَلَتْ حَتَّى إِذَا امْتَدَّتْ خَاصِرَتَاهَا اسْتَقْبَلَتْ عَيْنَ الشَّمْسِ، فَثَلَطَتْ وَبَالَتْ، وَرَتَعَتْ، وَإِنَّ هَذَا المَالَ خَضِرَةٌ حُلْوَةٌ، فَنِعْمَ صَاحِبُ المُسْلِمِ مَا أَعْطَى مِنْهُ المِسْكِينَ وَاليَتِيمَ وَابْنَ السَّبِيلِ - أَوْ كَمَا قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - وَإِنَّهُ مَنْ يَأْخُذُهُ بِغَيْرِ حَقِّهِ، كَالَّذِي يَأْكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ، وَيَكُونُ شَهِيدًا عَلَيْهِ يَوْمَ القِيَامَةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1465]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Yakwamba siku moja Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikaa juu ya Mimbari na tukakaa pembezoni mwake, akasema: "Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi kheri inaweza kuleta shari? Akanyamaza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakamwambia: Una nini wewe? Unamsemesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wala hakusemeshi? Tukamuona akiteremshiwa wahyi, anasema: akafuta jasho, akasema: "Yuko wapi muulizaji?" ni kana kwamba alipendezwa na swali lake, akasema: "Hakika kheri haileti shari, na hakika katika yale yanayooteshwa na masika huua au kudhuru, isipokuwa mifugo wanaokula malisho ya kijani, hula mpaka zinapopanuka mbavu zao hulielekea Jua, hujisaidia haja kubwa na ndogo, na wakapumzika, na hakika mali hii ni kijani kitamu, neema bora ya mtu muislamu ni ile aliyoitoa kumpa masikini na yatima na mpita njia -Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake- na hakika atakayeichukua pasina haki yake, ni sawa na yule anayekula wala hashibi na atakuwa shahidi juu ya mali hiyo siku ya Kiyama".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1465]
Alikaa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja juu Mimbari akiwahadithia Maswahaba zake akasema:
Hakika kikubwa ninachokihofia zaidi kwenu nyinyi baada yangu ni yale mtakayofunguliwa katika baraka za Ardhi na maua ya Dunia na pambo lake, na muonekano wake, na yale yaliyomo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na nguo na mazao na mengineyo miongoni mwa yale ambayo watu hujifaharisha kutokana na uzuri wake pamoja nakuwa yanadumu kwa muda mchache.
Mtu mmoja akasema: Maua ya Dunia ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, je inaweza kurudi neema hii na kuwa janga na adhabu?!
Watu wakamlaumu muulizaji pale walipomuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake kanyamaza, na wakadhania kuwa kamkasirisha.
Ikabainika kuwa rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiteremshiwa wahyi, kisha akaanza kufuta jasho katika paji lake la uso, akasema: Yuko wapi muulizaji?
Akasema: Mimi.
Akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kheri ya kweli haiji ila kwa kheri, lakini maua haya si kheri halisi kwa kuwa yanapelekea katika fitina na kushindana na kushughulika nayo na kuwacha kuielekea Akhera kikamilifu, kisha akapigia mfano wa hilo akasema: Hakika mimea ya masika na kijani chake; nayo ni aina za mimea ambazo huwapendeza sana wanyama, na huwaua kwa kuila kwa wingi na kuvimbewa au hukaribia kuwaua, isipokuwa mnyama anayekula mimea ya kijani aliyekula mpaka ikajaa sehemu ya tumbo lake, akaelekea juani na akatoa kinyesi chepesi kutoka tumboni mwake au akakojoa, kisha akayacheua yaliyoko tumboni mwake kisha akayatafuna kisha akayameza, kisha akarudi kula tena.
Hivyo mali hii ni kama majani ya kijani matamu, yanaua au yanakaribia kuuwa yanapokithiri; isipokuwa kama atatosheka na kidogo ambacho anahaja nacho na kitakachomtosha kwa njia ya halali, hii haidhuru, na neema bora ya muislamu ni kwa yule atakayetoa na kumpa masikini na yatima na mpitanjia, na yule mwenye kuichukua kwa haki atakabarikiwa katika mali hiyo, na atakayeichukua pasina haki yake mfano wake ni kama mfano wa yule anayekula wala hashibi, na mali hiyo itakuwa shahidi juu yake siku ya Kiyama.