عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله، مَنْ أحقُّ الناس بِحُسن صَحَابَتِي؟ قال: «أمك» قال: ثم مَنْ ؟ قال: «أمك»، قال: ثم مَنْ؟ قال: «أمك»، قال: ثم مَنْ؟ قال: «أبوك». متفق عليه. وفي رواية: يا رسول الله، مَنْ أحقُّ بحُسْنِ الصُّحْبَةِ؟ قال: «أمك، ثم أمك، ثم أمك، ثم أباك، ثم أدْنَاك أدْنَاك».
[صحيح] - [الرواية الأولى: متفق عليها. الرواية الثانية: رواها مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: "mama yako", akasema: kisha nani? akasema: "kisha mama yako" akasema: kisha nani? akasema: "kisha mama yako", akasema: kisha nani? akasema: "kisha baba yako",Hadithi Muttafaqun a'laihi. Na katika riwaya: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: "mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha nayemfuata kwa ukaribu".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Hadithi inaonyesha kuwa wazazi wote wawili wana haki ya kufanyiwa ukaribu mwema; na kuyajali kikamilifu mambo yao (Na uambatane nao katika dunia kwa wema), lakini haki ya mama iko juu ya haki ya baba kwa daraja nyingi, kwani hakutaja haki ya baba mpaka baada ya kuwa ametaja haki ya mama na akaisisitiza kikamilifu, kwa kutaja kwake mara tatu, bali cheo chake kimekuwa juu ya cheo cha baba pamoja nakuwa wanashrikiana katika kumlea mtoto, huyu kwa mali zake na uangalizi wake, na huyu kwa huduma zake katika kumlisha na kumnywesha na kumvisha na kumlaza, mpaka mwisho. Hii ni kwasababu mama ameumia kwaajili yake kwa mambo ambayo hakuumia nayo baba, kambeba miezi tisa tabu juu ya tabu, na udhaifu juu ya udhaifu; na akamzaa kwa shida; mpaka anakaribia kufa kwasababu ya misukosuko mikubwa anayokumbana nayo, na vile vile kamnyonyesha miaka miwili, anakesha ili yeye apate raha, anafanya kwaajili ya maslahi yake hata kama ataendelea kupata maumivu kwaajili ya hilo, na kwaajili hii wahyi ukatamka: (Na tumemuusia mwanadamu kwa wazazi wawili kuwafanyia wema, kambeba mama yake kwa tabu, na kamzaa kwa tabu, na kumbeba kwake na kumuachisha kwake (kunyonya) miezi thelathini), utaona kausiwa mwanadamu kwa wazazi wake wawili kuwafanyia wema; na hakueleza miongoni mwa sababu zaidi ya zile anazozipata mama ikiwa ni ishara ya ukubwa wa haki yake. Na katika uzuri wa kuishi na wazazi wawili ni kuwapa mahitaji ya chakula na kinywaji na mavazi; na mengineyo katika mahitajio ya kimaisha, ikiwa wanauhitaji, bali ikiwa wakiwa katika maisha ya chini au ya kati, nawe ukawa katika maisha ya neema na mazuri, basi wanyanyue katika daraja yako au zaidi, kwani hilo ni katika kuwafanyia wema na kuwa nao karibu. Na kumbuka alichokifanya Yusuf pamoja na wazazi wake akiwa tayari kapewa ufalme, pindi alipowanyanyua juu ya kiti cha ufalme baada yakuwa kawaleta kutoka kijijini. Na katika kuwafanyia wema, bali ndiyo jumla ya mambo yote, ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: (Na amehukumu Mola wako kuwa msiabudu ila yeye na wazazi wawili kuwafanyia wema, ikiwa atafikia kwako wewe utuuzima mmoja (kati yao) au wote wawili basi usiwaambie (hata) Aah! na wala usiwakaripie na useme nao kwa kauli nzuri. Na shusha kwao wao mbawa za unyenyekevu kwa huruma, na sema Mola wangu wahurumie kama walivyonilea mimi nikiwa mdogo" Zuia kwao ulimi wa uovu, na uwaepushie aina mbalimbali za maudhi. Na lainisha kwao kauli zako; na shusha kwaajili yao mbawa zako; na uidhalilishe kwaajili ya kuwatii nafsi yako, na uulowanishe ulimi wako kwa dua kwao toka moyoni mwako, na kwakukiri nafsini mwako, na sema: (Mola wangu wahurumie kama walivyonilea nikiwa mdogo), na wala usisahau ziada ya kipaumbele kwa mama, kwa kuifanyia kazi ishara iliyoonyeshwa katika wahyi; na kwa kuendana na kile kilichotamkwa katika hadithi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama