عن أسامة بن زيد بن حارثة رضي الله عنهما مرفوعًا: «يُؤتَى بِالرَّجُل يَومَ القِيَامَة فَيُلْقَى في النَّار، فَتَنْدَلِقُ أَقْتَاب بَطْنِه فَيدُورُ بِهَا كَمَا يَدُورُ الحِمَارُ فِي الرَّحَى، فَيَجْتَمِع إِلَيه أَهلُ النَّارِ، فَيَقُولُون: يَا فُلاَنُ، مَا لَكَ؟ أَلَم تَكُ تَأمُرُ بِالمَعرُوف وَتَنْهَى عَن المُنْكَر؟ فيقول: بَلَى، كُنتُ آمُرُ بِالمَعرُوف وَلاَ آتِيهِ، وَأَنهَى عَن المُنكَر وَآتِيهِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Usama bin zaidi bin Haritha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Ataletwa mtu siku ya kiyama atatupwa motoni, utatoka utumbo wa tumbo lake atazunguka nao kama punda anavyolizunguka jiwe la kusagia nafaka, watakusanyika kwake watu wa motoni, watasema: Ee fulani, una nini wewe? kwani hukuwa unaamrisha mema na unakataza mabaya? atasema: Ndivyo, nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza mabaya na ninayafanya".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Hadithi hii ndani yake kuna tahadhari kubwa ya mtu ambaye anaamrisha mema wala hayafanyi na anakataza maovu na anayafanya, na Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo. watamleta Malaika siku ya kiyama mtu atatupwa vibaya motoni, hatouingia taratibu, bali yeye atatupwa ndani yake kama linavyotupwa jiwe baharini, utatoka utumbo wake tumboni mwake kwasababu ya kutupwa vibaya, atazunguka na utumbo wake kama punda anavyozunguka katika jiwe la kusagia, watamkusanyikia watu wa motoni, watamwambia: Umekuwaje? ni kitu gani kimekuleta hapa, na wewe ulikuwa unaamrisha mema na kukataza mabaya? atasema akikiri mwenyewe kwa nafsi yake: Nilikuwa ninaamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza mabaya na ninayafanya, jambo la msingi kwa mtu aanze na nafsi yake aiamrishe mema na aikataze mabaya; kwasababu katika watu wenye haki kubwa zaidi kwako baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni nafsi yako.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama