عَن الحَسَنِ قال: حَدَّثنا جُنْدَبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنه، فِي هَذَا المَسْجِدِ، وَمَا نَسِينَا مُنْذُ حَدَّثَنَا، وَمَا نَخْشَى أَنْ يَكُونَ جُنْدُبٌ كَذَبَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلّى الله عليه وسلم:
«كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ رَجُلٌ بِهِ جُرْحٌ، فَجَزِعَ، فَأَخَذَ سِكِّينًا فَحَزَّ بِهَا يَدَهُ، فَمَا رَقَأَ الدَّمُ حَتَّى مَاتَ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: بَادَرَنِي عَبْدِي بِنَفْسِهِ، حَرَّمْتُ عَلَيْهِ الجَنَّةَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3463]
المزيــد ...
Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3463]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.