عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِذِي الحُلَيْفَةِ، فَأَصَابَ النَّاسَ جُوعٌ، فَأَصَابُوا إِبِلًا وَغَنَمًا، قَالَ: وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أُخْرَيَاتِ القَوْمِ، فَعَجِلُوا، وَذَبَحُوا، وَنَصَبُوا القُدُورَ، فَأَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالقُدُورِ، فَأُكْفِئَتْ، ثُمَّ قَسَمَ، فَعَدَلَ عَشَرَةً مِنَ الغَنَمِ بِبَعِيرٍ فَنَدَّ مِنْهَا بَعِيرٌ، فَطَلَبُوهُ، فَأَعْيَاهُمْ وَكَانَ فِي القَوْمِ خَيْلٌ يَسِيرَةٌ، فَأَهْوَى رَجُلٌ مِنْهُمْ بِسَهْمٍ، فَحَبَسَهُ اللَّهُ، ثُمَّ قَالَ: «إِنَّ لِهَذِهِ البَهَائِمِ أَوَابِدَ كَأَوَابِدِ الوَحْشِ، فَمَا غَلَبَكُمْ مِنْهَا فَاصْنَعُوا بِهِ هَكَذَا»، فَقَالَ أي رافع: إِنَّا نَرْجُو -أَوْ نَخَافُ- العَدُوَّ غَدًا، وَلَيْسَتْ مَعَنَا مُدًى، أَفَنَذْبَحُ بِالقَصَبِ؟ قَالَ: «مَا أَنْهَرَ الدَّمَ، وَذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ فَكُلُوهُ، لَيْسَ السِّنَّ وَالظُّفُرَ، وَسَأُحَدِّثُكُمْ عَنْ ذَلِكَ: أَمَّا السِّنُّ فَعَظْمٌ، وَأَمَّا الظُّفُرُ فَمُدَى الحَبَشَةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2488]
المزيــد ...
Kutoka kwa Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake maeneo ya Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, wakapata ngamia na mbuzi, akasema: Na Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mwisho wa watu wote, wakaharakisha, wakachinja, na wakabandika vyungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha vyungu vikamiminwa, kisha akagawa na akalinganisha mbuzi kumi sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja akatoroka, wakamtafuta, akawashinda, na hawakuweza kumpata, na walikuwa na farasi wachache, mtu mmoja akarusha mshale, Mwenyezi Mungu akauzuia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wanyama hawa wafugwao ni wanyama kama walivyo wanyama pori, watakaokushindeni miongoni mwao (kuwachinja) basi fanyeni hivyo", Raafi akasema: Sisi tunawahofia maadui kesho, na hatuna visu, je tuchinje kwa miti mikavu iliyochongwa? Akasema: "Mnyama yoyote atakayemwagwa damu, na akatajiwa jina la Mwenyezi Mungu basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuelezeni kuhusu hilo: Ama jino ninamaanisha mfupa, na ama kwato ni visu vya wahabeshi".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2488]
Ameeleza Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake eneo la Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, na walikuwa wamepata ngawira kutoka kwa washirikina, ngamia pamoja na mbuzi, wakafanya haraka kabla ngawira hazijagawanywa wakazichinja, na wakabandika vyungu jikoni, pasina ya kumuomba idhini Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitembea mwishoni mwa watu, alipojua hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha vyungu vikamiminwa pamoja na mchuzi wake, kisha akawagawia ngawira baina yao, akafanya mbuzi kumi ni sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja katika hao akakimbia, wakashindwa kumkamata wala kumpata, na farasi walikuwa wachache, bwana mmoja akampiga yule ngamia kwa mshale, Mwenyezi Mungu akawazuilia, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika wanyama hawa wafugwao wana tabia kama tabia za wanyama pori, watakapokushindeni miongoni mwao na hamkuweza kuwakamata basi fanyeni hivyo. Akasema Raafi: Hakika sisi tunataraji kukutana na maadui zetu kesho na tunahofia kuharibu makali ya silaha zetu ikiwa tutazichinjia, na tunahaja kubwa ya kuchinja, na hatuna kisu, je tuchinje kwa miti ya mwanzi mikavu? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kitakachomwaga damu na kikaitiririsha na kikaimwaga kwa wingi, na likatajwa jina la Mwenyezi Mungu, basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuhadithieni kuhusu hilo: Ama jino ni mfupa, na ama kwato hizo makafiri wa Ethiopia huzitumia.