عن حُذَيْفَةَ بْنِ الْيَمَانِ رضي الله عنهما مرفوعاً: «لا تلْبَسُوا الحرير ولا الديباج، ولا تشربوا في آنية الذهب والفضة ولا تأكلوا في صِحَافِهِمَا؛ فإنَّهَا لهم في الدنيا ولكم في الآخرة».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Hudhaifa bin Yamani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Msivae hariri nyepesi wala nguo zilizofumwa kwa hariri, na wala msinywe katika vyombo vya dhahabu wala fedha, na wala msile katika sahani zake, kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyenu Akhera".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Amewakataza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- wanaume kuvaa hariri na dibaji (nguo zilizofumwa kwa hariri); kwa kile kinachopatikana kwa mwanaume katika kuvivaa miongoni mwa ulaini na kuiga tabia za kike, na kujifananisha na wanawake wenye kujiremba na wenye anasa. Na mwanaume anatakiwa kuwa na ugumu ukakamavu. Kama alivyowakataza wote wanawake na wanaume kula na kunywa katika sahani za dhahabu na fedha na vyombo vyake; Na hekima yake kama alivyosema -Rehema na Amani ziwe juu yake: Nikuwa kulia ndani yake hapa duniani ni kwaajili ya makafiri ambao wameviharakisha vizuri vyao katika maisha yao ya dunia, na wakastareheka navyo, Navyo ni vyenu maalumu -enyi waislamu- siku ya kiyama mtakapoviepuka; kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- Na kwa kutamani yale yaliyoko kwake, kwa kukatazwa kujifananisha nao na kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu -Mtukufu- vikaharamishwa. kama jinsi ambavyo atakayevaa hariri katika wanaume duniani atakuwa kaharakisha starehe yake; na kwaajili hiyo basi yeye hatoivaa akhera, Na mwenye kuharakisha jambo kabla ya wakati wake tena kwa njia ya haramu basi anaadhibiwa kwa kumnyima jambo hilo, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo الدرية
Kuonyesha Tarjama