عَنْ عُمَرَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ لَبِسَ الحَرِيرَ فِي الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ فِي الآخِرَةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5834]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5834]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.