+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَحَاسَدُوا، وَلَا تَنَاجَشُوا، وَلَا تَبَاغَضُوا، وَلَا تَدَابَرُوا، وَلَا يَبِعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إِخْوَانًا الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يَخْذُلُهُ، وَلَا يَحْقِرُهُ التَّقْوَى هَاهُنَا» وَيُشِيرُ إِلَى صَدْرِهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ «بِحَسْبِ امْرِئٍ مِنَ الشَّرِّ أَنْ يَحْقِرَ أَخَاهُ الْمُسْلِمَ، كُلُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ حَرَامٌ، دَمُهُ، وَمَالُهُ، وَعِرْضُهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2564]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
" Msihusudiane, na wala msipandishiane bei, na wala msichukiane, na wala msitengane, na wala wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu muislamu ni ndugu wa muislamu, asimdhulumu, na wala asimsaliti, na wala asimdharau, ucha Mungu uko hapa" Na huku akiashiria katika kifua chake mara tatu "Yamtosha mtu kuwa ni shari kwake kwa kumdharau ndugu yake muislamu, kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu damu yake, na mali yake, na heshima yake".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2564]

Ufafanuzi

Alimuusia Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kwa ndugu yake muislamu kumtendea mazuri, na akabainisha baadhi ya yale yanayomlazimu katika wajibu na adabu kwao; na miongoni mwa hayo: Wasia wa kwanza: Msihusudiane kwa kutamani baadhi yenu neema za wengine ziwaondokee. Wa pili: Wala msipandishiane, kwa kuzidisha katika bidhaa hali yakuwa hana nia ya kununua; isipokuwa anataka kumnufaisha muuzaji, au kumdhuru mnunuzi. Ya tatu: Msichukiane; nako ni kutaka kuleta madhara, kitu ambacho ni kinyume na mapenzi; isipokuwa kuchukiana kutakapokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; hapo ni wajibu. Ya nne: Msitengane, nako ni kila mmoja miongoni mwenu kumpa mgongo na kisogo ndugu yake, na akampuuza na kumhama. Ya tano: Wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, kwa mtu kumwambia aliyenunua bidhaa: Nina bidhaa kama hiyo kwa bei nafuu kuliko hiyo, au nina bidhaa bora kuliko hiyo na kwa bei hiyo hiyo. Kisha akausia rehema na amani ziwe juu yake kwa usia wa ujumla, akasema: Na kuweni kama ndugu kwa kuyaacha yaliyotajwa katika makatazo, na kwa kujitolea mapenzi na huruma na upole na kusikilizana na kusaidizana katika mambo ya kheri, ikiwa ni pamoja na kusafisha mioyo na kunasihiana kwa kila hali. Na miongoni mwa mambo yanayojenga udugu huu: Asimdhulumu ndugu yake muislamu na wala asimfanyie uadui. Na wala asiache ndugu yake muislamu akadhulumiwa akamsaliti katika mahali ambapo anaweza kumtetea na akapata haki yake, na akamuondolea dhulma. Na asimdharau na akamuona duni na akamtazama kwa jicho la kumshusha thamani na kumkejeli; na hilo ni matokeo ya kiburi kilichopo ndani ya moyo. Kisha akabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara tatu kuwa ucha Mungu uko moyoni, na atakayekuwa na ucha Mungu ndani ya moyo wake unaopelekea katika tabia njema, na kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumchunga, basi hawezi kumdharau muislamu, na yamtosha kwake kuwa na mambo ya shari na tabia chafu kwa kumdharau ndugu yake muislamu; na hilo ni kwa sababu ya kiburi kilichopo moyoni mwake. Kisha akasisitiza rehema na amani ziwe juu yake hayo yaliyopita kuwa kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu: Damu yake: Kwa kumfanyia uadui akamuuwa, au chini ya hapo kama kumjeruhi au kumpiga na mfano wake, na vile vile mali yake: Kwa kuichukuwa pasina haki, na vile vile heshima yake: Kwa kumtukana yeye mwenyewe au ukoo wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amri ya kutekeleza jambo lolote linalopelekea udugu wa kiimani, na katazo la kufanya kinyume chake miongoni mwa kauli na vitendo.
  2. Nguzo ya ucha Mungu ndani ya moyo ni kumtambua Mwenyezi Mungu, na kumuogopa na kumchunga, una ucha Mungu huu ndio unaozaa matendo mema.
  3. Kupinda kwa wazi kunaonyesha udhaifu wa ucha Mungu wa moyo.
  4. Katazo la kumuudhi muislamu kwa aina yoyote ile, kwa kauli au kitendo.
  5. Si katika husuda muislamu kutamani awe kama mwenzake, bila kutamani neema hiyo iondoke kwa mwenzake, na hii huitwa kufurahia neema ya mwenzio (na kuitamani pia uipata); na hii inafaa, kwani inasaidia watu kushindana katika mambo ya kheri.
  6. Mwanadamu katika tabia zake hapendi yeyote amzidi katika chochote miongoni mwa fadhila, ikiwa atapenda iondoke neema hiyo kwa mwenzake hiyo itakuwa ni husuda mbaya, na ikiwa atapenda kushindana basi hiyo inaitwa kufarahia neema kunako faa.
  7. Si katika kuuza muislam juu ya biashara ya ndugu yake kwa kumuweka wazi mteja kuwa kadanganywa katika kununua tena uongo mbaya; bali hili ni katika sehemu ya nasaha, kwa sharti iwe matokeo yake ni kumnasihi ndugu yake mnunuzi, na si kumdhuru muuzaji, kwani matendo huhukumiwa kwa nia.
  8. Si katika kuuza muislamu juu ya biashara ya ndugu yake ikiwa muuzaji na mnunuzi hawajakubaliana na wala kiwango cha thamani hakijapitishwa.
  9. Si katika kuchukiana kuliko katazwa ndani ya hadithi: Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bali hilo ni wajibu, na ni katika misingi mizito ya imani.