عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2759]
المزيــد ...
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2759]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.