عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَمَّا عُرِجَ بِي مَرَرْتُ بِقَوْمٍ لَهُمْ أَظْفَارٌ مِنْ نُحَاسٍ يَخْمُشُونَ بها وُجُوهَهُمْ وَصُدُورَهُمْ، فَقُلْتُ: مَنْ هَؤُلَاءِ يَا جِبْرِيلُ، قَالَ: هَؤُلَاءِ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ لُحُومَ النَّاسِ، وَيَقَعُونَ فِي أَعْرَاضِهِمْ».
[حسن] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 4878]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao, nikasema: Ni akina nani hao ewe Jibrili, akasema: Hawa ni wale wanaokula nyama za watu, na wanajitumbukiza katika kuvunja heshima za watu".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad] - [سنن أبي داود - 4878]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba yeye pindi alipopandishwa juu mbinguni usiku Israa na Miiraji (safari ya usiku na kupandishwa), alipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba wakizikwarua na kuzichana kwazo nyuso zao na vifua vyao, akamuuliza rehema na amani ziwe juu yake Jibril amani iwe juu yake: Ni kitu gani walifanya hawa mpaka wanalipwa kwa adhabu hii? Akasema Jibril amani iwe juu yake: Hawa ni wale wanaosengenya watu, na wanazungumza vibaya kuhusu heshima zao pasina haki.