+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ سمعتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يقولُ:
«أَلاَ إِنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا، إِلاَّ ذِكْرُ اللهِ وَمَا وَالاَهُ وَعَالِمٌ أَوْ مُتَعَلِّمٌ».

[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2322]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi".

[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 2322]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba dunia na vilivyomo inachukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu na haipendezi bali imetengwa mbali, yameachwa yote yaliyomo hayasifiki kwa uzuri; kwakuwa dunia na vilivyomo hushughulisha na kuwatenga mbali watu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kila kinachokaribia hilo na kuwa katika aina hiyo katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu, au mwalimu wa elimu ya kisheria anayewafundisha watu, au mwenye kujifunza.

Katika Faida za Hadithi

  1. Haifai kuilaani dunia kwa ujumla; kwa kunukuliwa hadithi zinazokataza hilo, lakini inafaa kuyaalani yale yanayomfanya mtu kuwa mbali na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumshughulisha mtu na kumtii Mwenyezi Mungu.
  2. Yote yaliyomo duniani ni mchezo na ni upuuzi isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayokuwa sababu na kisaidizi cha hilo.
  3. Kumebainishwa fadhila za elimu na wasomi wake na wanafunzi wake.
  4. Amesema bin Taimia: Bali husemwa vibaya yale ya haramu yaliyopatikana pasina njia nzuri, au halali iliyokuja kwa mfumo wa wingi na kujifaharisha, na yanayolimbikizwa kwa lengo la kujigamba na kujitapa, haya ndio yanayochukiwa kwa mwenye akili.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama