عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَقِيتُ إِبْرَاهِيمَ لَيْلَةَ أُسْرِيَ بِي فَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَقْرِئْ أُمَّتَكَ مِنِّي السَّلاَمَ، وَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ الجَنَّةَ طَيِّبَةُ التُّرْبَةِ عَذْبَةُ الْمَاءِ، وَأَنَّهَا قِيعَانٌ، وَأَنَّ غِرَاسَهَا سُبْحَانَ اللهِ وَالحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ».
[حسن بشواهده] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3462]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake-:
"Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam, nakuwa imenyooka na kulingana sawa, nakuwa mimea yake: ni (kusema) Sub-haana llaah -Ametakasika Mwenyezi Mungu, Na Alhamdulillaah -Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Na Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Allaahu Akbar -Mwenyezi Mungu Mkubwa".
- [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 3462]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa alikutana na Ibrahim mwandani amani iwe juu yake usiku aliposafirishwa kwenda mbinguni (Israa wal Miiraji), akasema kumwambia: Ewe Muhammadi: Wafikishie umma wako kutoka kwangu salamu, na ulijulishe kuwa Pepo ina udongo mzuri, ina maji matam yasiyokuwa na chumvi, na kuwa Pepo ni pana, ni tambarare haina miti, na kuipanda kwake ni kwa maneno mazuri, nayo ni mema yenye kubakia: Sub-haanallaah, Alhamdulillaah, wa Laa ilaaha illa llaah, wallaahu Akbaru, kila anapoyasema muislamu na kuyarudiarudia hupandia mmea Peponi.