عن أبي هريرة ـ رضي الله عنه ـ قال: سمعت رسول الله -صلى الله عليه وسلم- يقول: «لم يبقَ من النُّبُوَّةِ إلا المُبَشِّرَاتُ» قالوا: وما المُبَشِّرَاتُ ؟ قال: «الرؤيا الصالحة».
[صحيح.] - [رواه البخاري.]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: "Haijabakia katika utume isipokuwa viashiria vya habari njema" wakasema: ni vipi hivyo viashiria? Akasema: "Ni ndoto njema".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Anaashiria Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa ndoto njema ndio viashiria, nazo ndiyo athari za utume zilizobakia baada ya kukatika kwa wahyi, na hayajabakia yanayoweza kutumika kujua mambo yatakayotokea isipokuwa ndoto njema.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama