+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لو كان لي مِثْلُ أحدٍ ذهبًا، لسرني أن لا تمر عليَّ ثلاث ليالٍ وعندي منه شيءٌ إلا شيء أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ».
[صحيح] - [متفق عليه واللفظ للبخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-Amesema: "Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la Bukhaariy]

Ufafanuzi

Lau kama ningekuwa ninamiliki katika mali kiasi cha dhahabu halisi kama mlima Uhudi, basi ningekitoa chote katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nisingebakisha katika mali hiyo ila kiasi ninachokihitaji kwa kukidhi mahitaji, na kulipa madeni ninayodaiwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama