عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ، مَا لاَ عَيْنٌ رَأَتْ، وَلاَ أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلاَ خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ» قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: اقْرَؤُوا إِنْ شِئْتُمْ: {فَلاَ تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ} [السجدة: 17].
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4779]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote" Akasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Basi nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajida: 17).
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4779]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema: Nimetayarisha na nimeandaa kwa ajili ya kuwatukuza waja wangu wema peponi mambo ambayo uhalisia wake hakuna jicho liliwahi kuona, na wala sikio lolote kusikia wasifu wake, wala kutokea wala kupita ndani ya moyo wa binadamu yeyote uhalisia wake. Akasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Someni mkitaka:
"Nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajda: 17]