عَنِ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها زَوْجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
أَنَّ الْحَوْلَاءَ بِنْتَ تُوَيْتِ بْنِ حَبِيبِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى مَرَّتْ بِهَا وَعِنْدَهَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: هَذِهِ الْحَوْلَاءُ بِنْتُ تُوَيْتٍ، وَزَعَمُوا أَنَّهَا لَا تَنَامُ اللَّيْلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَنَامُ اللَّيْلَ! خُذُوا مِنَ الْعَمَلِ مَا تُطِيقُونَ، فَوَاللهِ لَا يَسْأَمُ اللهُ حَتَّى تَسْأَمُوا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 785]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
Ya kwamba Haulaa binti Tuwaiti bin Habib bin Asadi bin Abdil-Uzza, alipita kwake akiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikasema: Huyu hapa Haulaa binti Tuwaiti, na wanadai kuwa huwa halali usiku, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake (kwa mshangao): "Halali usiku! hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 785]
Alikuwa kwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Haulaa bin Tuwaiti radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akatoka alipoingia tu Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Aisha akasema kumwambia: Mwanamke huyu halali usiku, bali hukesha kwa kuswali. Akasema rehema na amani ziwe juu yake akipinga kijitiadhiki kwa mwanamke huyo juu ya nafsi yake: Halali usiku! Hebu shughulikeni na matendo mema kwa kiasi mnachoweza kudumu nacho, namuapa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hachoki kuwapa waja wake wema wenye kumtii thawabu na malipo kwa utiifu wao na mema yao na amali zao njema mpaka wachoke na waache kufanya amali.