عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ:
«اللهُمَّ لَا عَيْشَ إِلَّا عَيْشُ الْآخِرَهْ، فَاغْفِرْ لِلْأَنْصَارِ وَالْمُهَاجِرَهْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1805]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1805]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hakuna maisha halisi isipokuwa maisha ya Akhera katika radhi za Mwenyezi Mungu na rehema zake na pepo yake; kwa sababu maisha ya Dunia huondoka, na maisha ya Akhera ndio ya kudumu na kubakia, kisha akawaombea msamaha na ukarimu na kutengemaa rehema na amani ziwe juu yake Maanswari wale waliompa makazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja Muhajirina wale walioacha miji yao na mali zao wakitafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake.