عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: "لا عَدْوَى ولا طِيَرَة ولا هَامَةَ ولا صَفَرَ" أخرجاه. زاد مسلم "ولا نَوْءَ ولا غُولَ".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, wala mkosi wa Bundi,na aina zingine za ndege,wala kutuhumu kuwa mwezi wa safari unamikosi, au maradhi ya tumbo yanayompata ngamia. wameitoa hadithi hii Maimamu wawili (Bukhariy na Muslim). Akaongeza Muslim "Na wala hakuna mikosi ya nyota wala hakuna Ghulu (Jamii ya majini).
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Ilikuwa zama za ujinga zimezungukwa na mambo ya hovyo na dhana ambazo hazikuegemezwa katika ushahidi wowote, ukataka uislamu uwakinge wafuasi wake na mambo hayo ya batili, ukayapinga yale waliyokuwa wakiyaamini washirikina katika vitu hivi vilivyotajwa katika hadithi, baadhi vimepingwa uwepo wake kabisa kama imani ya mikosi ya ndege, na baadhi yake imepingwa kuathiri kwake yenyewe binafsi; kwasababu hakuna aletaye mazuri ila Mwenyezi Mungu na hakuna azuiaye mabaya isipokuwa yeye.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama