+ -

عَن هَانِئ مَوْلَى عُثْمَانَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كَانَ عُثْمَانُ إِذَا وَقَفَ عَلَى قَبْرٍ بَكَى حَتَّى يَبُلَّ لِحْيَتَهُ، فَقِيلَ لَهُ: تُذْكَرُ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَلَا تَبْكِي، وَتَبْكِي مِنْ هَذَا؟ فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
«إِنَّ الْقَبْرَ أَوَّلُ مَنْزِلٍ مِنْ مَنَازِلِ الْآخِرَةِ، فَإِنْ نَجَا مِنْهُ فَمَا بَعْدَهُ أَيْسَرُ مِنْهُ، وَإِنْ لَمْ يَنْجُ مِنْهُ فَمَا بَعْدَهُ أَشَدُّ مِنْهُ».

[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2308]
المزيــد ...

Kutoka kwa Haani, mwachwa huru wa Othmani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Othmani anaposimama juu ya kaburi analia mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Ukikumbuka pepo na Moto wala haulii, na unalia kwa sababu ya hili (kaburi)?! Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema:
"Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili".

[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 2308]

Ufafanuzi

Alikuwa kiongozi wa waumini Othmani bin Affani radhi za Allah ziwe juu yake anaposimama juu ya kaburi analia sana, mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Unakumbuka pepo na moto na wala haulii kwa shauku ya pepo wala hofu ya moto! na unalia kwa sababu ya kaburi? Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza kuwa hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, mtu akisalimika na akaepukana na mabaya yaliyomo basi vituo vinavyofuata baada yake ni vyepesi mno, na asiposalimika kutokana na adhabu zake; basi adhabu zinazofuata baada yake ni kali kuliko hizo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Thai Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa hofu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyokuwa nayo Othmani radhi za Allah ziwe juu yake, pamoja nakuwa yeye ni miongoni mwa waliobashiriwa pepo.
  2. Sheria ya kulia wakati wa kukumbuka misukosuko ya kaburi na Kiyama.
  3. Kumethibitishwa neema za kaburi na adhabu zake.
  4. Tishio la adhabu za kaburi.