+ -

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«الحَسَن والحُسَيْن سَيِّدا شَباب أهْل الجنة».

[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 3768]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 3768]

Ufafanuzi

Alieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hapa kuna fadhila za wazi za Hassan na Hussein radhi za Allah ziwe juu yao.
  2. Imesemekana katika maana ya hadithi kuwa: Wao wakati wa kuzungumzwa hadithi hii walikuwa ndio mabosi wa vijana wa wale miongoni mwao watakaokuwa katika watu wa peponi katika vijana wa zama hizi, au wao ni bora kuliko yule ambaye fadhila zake hazijathibiti kwa ujumla kama Manabii na Mahalifa (viongozi), au wao ni mabosi wa kila mwenye kusifika na sifa ya ujana, kama murua (heshima) na ukarimu na ushujaa, na haukutajwa umri maalumu wa ujana; kwa sababu Hassan na Hussein walikufa wakiwa watu wazima.