عن أنس رضي الله عنه، قال:
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لأبي بكر وعمر: «هذان سَيِّدا كُهُول أهل الجنة من الأوَّلِين والآخِرين إلا النبيِّين والمرسلين».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3664]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 3664]
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.